Ewostatewos

Ewostatewos (kwa Kigeez: ኤዎስጣቴዎስ, ʾĒwōsṭātēwōs, au ዮስጣቴዎስ, Yōsṭātēwōs, kutoka Kigiriki Εὐστάθιος, Eustathios; 15 Julai 127315 Septemba 1352 kadiri ya Kalenda ya Juliasi) alikuwa mmonaki, mwalimu wa Absadi.

Alidai utekelezaji wa Sabato pamoja na Dominika katika Ukristo wa Ethiopia. Hatimaye wafuasi wake walifaulu kufanya msimamo huo ukubaliwe mwaka 1450 kwenye Mtaguso wa Debre Mitmaq huko Tegulet.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia na Kanisa la Kiorthodoksi la Eritrea kama mtakatifu.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy