Fara

Mt. Fara katika dirisha la kioo cha rangi.

Fara (Poincy, karne ya 6 - Faremoutiers, 675) alikuwa mwanzilishi na abesi wa kwanza wa monasteri wa Faremoutiers nchini Ufaransa kwa miaka 40[1].

Ndiye aliyemfanya kaka yake, Faro amhimize mke wake kujiunga na monasteri ili yeye aingie upadri.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu bikira.

Sikukuu yake ni tarehe 7 Desemba[2].

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/90270
  2. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy