Kianuak

Kianuak ni lugha ya Kinilo-Sahara nchini Ethiopia na Sudan Kusini inayozungumzwa na Waanuak. Mwaka wa 2007 idadi ya wasemaji wa Kianuak nchini Ethiopia imehesabiwa kuwa watu 88,000. Nchini Sudan Kusini kuna wasemaji 52,000 (1991). Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kianuak iko katika kundi la Kinilotiki.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy