Kidijim-Bwilim

Kidijim-Bwilim ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Nigeria inayozungumzwa na Wadijim na Wabwilim. Dijim na Bwilim ni majina ya lahaja mbili za lugha hiyo moja. Mwaka wa 1998 idadi ya wasemaji wa Kidijim-Bwilim imehesabiwa kuwa watu 25,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kidijim-Bwilim iko katika kundi la Kiadamawa-Ubangi.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy