Kidusun-Malang

Kidusun-Malang ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wadusun na Wabayan kwenye kisiwa cha Kalimantan. Mwaka wa 2003 idadi ya wasemaji wa Kidusun-Malang imehesabiwa kuwa watu 4500, yaani Wadusun 2500 na Wabayan 2000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kidusun-Malang iko katika kundi la Kibarito.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy