Kihawu

Kihawu (pia Kisawu) ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wahawu kwenye visiwa vya Sawu, Raijua, Sumba na Flores. Pia Wahawu wengine wamehamia kisiwa cha Timor. Mwaka wa 1997 idadi ya wasemaji wa Kihawu imehesabiwa kuwa watu 110,000 ambao 30,000 wao huishi nje ya eneo la lugha. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kihawu iko katika kundi la Kisumba-Hawu.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy