Kiholma

Kiholma ilikuwa lugha ya Kiafrika-Kiasia nchini Nigeria iliyozungumzwa na Waholma. Hakuna wasemaji wa Kiholma wabakio kwa vile wote wamebadili lugha yao kuwa Kifulfulde siku hizi. Maana yake, lugha ya Kiholma imetoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiholma iko katika kundi la Kichadiki.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy