Kihu

Kihu ni lugha ya Kiaustro-Asiatiki nchini Uchina inayozungumzwa na Wahu. Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kihu imehesabiwa kuwa watu 1000. Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kihu iko katika kundi la Kipalaungiki. Wengine huiangalia kuwa sawa na lugha ya Kikon-Keu.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy