Kihukumina

Kihukumina (pia Kibambaa) ilikuwa lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia iliyozungumzwa na Wahukumina kwenye kisiwa cha Buru. Hakuna watu wanaojulikana kuongea lugha ya Kihukumina, maana yake lugha imetoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kihukumina iko katika kundi la Kimalayo-Polinesia kama lugha nyingi za Kiaustronesia; haiwezekani kuiainisha kwa usahihi zaidi.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy