Kijilbe

Kijilbe ni lugha ya Kiafrika-Kiasia nchini Nigeria inayozungumzwa na Wajilbe. Mwaka wa 1999 idadi ya wasemaji wa Kijilbe imehesabiwa kuwa watu 100 tu. Kwa hiyo inawezekana kuwa lugha ya Kijilbe itatoweka hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kijilbe iko katika kundi la Kichadiki.


From Wikipedia, the free encyclopedia ยท View on Wikipedia

Developed by Tubidy