Kikalenjin

Kikalenjin ni lugha za Kinilo-Sahara zinazozungumzwa na Wakalenjin nchini Kenya. Mwaka wa 2009 idadi ya wasemaji wa Kikalenjin ilihesabiwa kuwa zaidi ya watu milioni 5. Kufuatana na uainishaji wa lugha wa ndani zaidi, Kikalenjin kiko katika kundi la Kiniloti.

Miongoni mwa lugha za Kikalenjin ni Kikeiyo, Kikipsigis, Kimarkweeta, Kinandi, Kiokiek, Kipokoot, Kisabaot, Kiterik na Kitugen.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy