Kikuri

Kikuri (pia Kimodan au Kinabi) ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wakuri kwenye kisiwa cha Papua. Mwaka wa 1982 idadi ya wasemaji wa Kikuri imehesabiwa kuwa watu 500 tu. Kwa vile Wakuri wengi wameacha lugha yao, Kikuri iko hatarini mwa kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha Kikuri haijaainishwa kwa ndani zaidi.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy