Kilama

Kilama ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Togo na Benin inayozungumzwa na Walama. Mwaka wa 1991 idadi ya wasemaji wa Kilama nchini Togo imehesabiwa kuwa watu 117,000. Pia kuna wasemaji 60,000 nchini Benin na wasemaji wachache nchini Ghana. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kilama iko katika kundi la Kigur.


From Wikipedia, the free encyclopedia ยท View on Wikipedia

Developed by Tubidy