Kimajera

Kimajera ni lugha ya Kiafrika-Kiasia nchini Kamerun na Chad inayozungumzwa na Wamajera. Mwaka wa 2004 idadi ya wasemaji wa Kimajera nchini Kamerun imehesabiwa kuwa watu 500 tu. Lakini mwaka wa 2002 wataalamu wengine wamehesabu wasemaji 2300 wa Kimajera ambao nusu wamekaa nchini Chad. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimajera iko katika kundi la Kichadiki.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy