Kinda'nda'

Kinda'nda' ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Kamerun inayozungumzwa na Wanda'nda'. Mwaka wa 1990 idadi ya wasemaji wa Kinda'nda' imehesabiwa kuwa watu 10,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kinda'nda' iko katika kundi la Grassfields ambalo linafanana na lugha za Kibantu.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy