Kingombale

Kingombale ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Kamerun inayozungumzwa na Wangombale. Mwaka wa 1993 idadi ya wasemaji wa Kingombale imehesabiwa kuwa watu 45,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kingombale iko katika kundi la Grassfields ambalo linafanana na lugha za Kibantu.


From Wikipedia, the free encyclopedia ยท View on Wikipedia

Developed by Tubidy