Kingwana

Kingwana ni lahaja ya Kiswahili inayozungumzwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, hasa upande wa mashariki.

Chanzo cha Kingwana ni Kiswahili cha wafanyabiashara na askari kutoka pwani ya Bahari Hindi (leo nchini Tanzania) walioingia katika Katanga kwa biashara ya watumwa na pembe za ndovu wakati ya karne ya 19 kabla ya ukoloni.

Lugha ikaendelea ilipokuwa chombo cha mawasiliano katika mchanganyiko wa watu wa makabila mbalimbali walioelekea kutafuta kazi katika migodi ya Katanga na Kongo ya Mashariki.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy