Kinzanyi

Kinzanyi ni lugha ya Kiafrika-Kiasia nchini Nigeria na Kamerun inayozungumzwa na Wanzanyi. Mwaka wa 1993 idadi ya wasemaji wa Kinzanyi nchini Nigeria imehesabiwa kuwa watu 77,000. Pia kuna wasemaji 9000 nchini Kamerun. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kinzanyi iko katika kundi la Kichadiki.


From Wikipedia, the free encyclopedia ยท View on Wikipedia

Developed by Tubidy