Kipapel

Kipapel ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Guinea-Bisau na Senegal inayozungumzwa na Wapapel. Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kipapel nchini Guinea-Bisau imehesabiwa kuwa watu 136,000. Pia kuna wasemaji 4200 nchini Senegal. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kipapel iko katika kundi la Kiatlantiki.


From Wikipedia, the free encyclopedia ยท View on Wikipedia

Developed by Tubidy