Kipunu

Kipunu ni lugha ya Kibantu nchini Gabon na jamhuri ya Kongo inayozungumzwa na Wapunu. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kipunu nchini Gabon imehesabiwa kuwa watu 123,000. Pia kuna wasemaji zaidi ya 9000 nchini Kongo. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kipunu iko katika kundi la B40.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy