Kipyu

Kipyu ni lugha nchini Papua Guinea Mpya inayozungumzwa na Wapyu. Isichanganywe na lugha ya Kipiu ambayo ni lugha ya Kiaustronesia. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kipyu imehesabiwa kuwa watu 100. Kwa vile Wapyu wengi wameanza kuacha lugha yao, Kipyu iko hatarini mwa kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kipyu iko peke yake, yaani hailingani wala kuhusiana na lugha wala kundi la lugha nyingine yoyote.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy