Kiseki

Kiseki ni lugha ya Kibantu nchini Guinea ya Ikweta na Gabon inayozungumzwa na Waseki. Mwaka wa 2001 idadi ya wasemaji wa Kiseki nchini Guinea imehesabiwa kuwa watu 11,000. Pia kuna wasemaji 3690 nchini Gabon. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kiseki iko katika kundi la B20.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy