Kisinyar

Kisinyar ni lugha ya Kinilo-Sahara nchini Chad inayozungumzwa na Wasinyar. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kisinyar nchini Chad imehesabiwa kuwa watu 12,300. Pia kuna Wasinyar nchini Sudan lakini haijulikani kama wameendelea kuongea Kisinyar. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kisinyar iko katika kundi la Kibongo-Bagirmi.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy