Kiwawonii

Kiwawonii ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wawawonii kwenye visiwa vya Wawonii na Menui. Mwaka wa 2004 idadi ya wasemaji wa Kiwawonii imehesabiwa kuwa watu 30,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiwawonii iko katika kundi la Kicelebiki.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy