Kiwikngenchera

Kiwikngenchera (pia Kiwik-Nantjara au Kikugu-Nganhcara) ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wawik katika jimbo la Queensland. Mwaka wa 2005, idadi ya wasemaji wa Kiwikngenchera ilihesabiwa kuwa watu 30 tu, na wasemaji wengi wameacha lugha yao ya kwanza na kutumia Kiwik-Mungkan. Kwa hiyo, Kiwikngenchera imo hatarini mwa kutoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiwikngenchera kiko katika kundi la Kipama cha Kati.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by razib.in