Kiyei

Kiyei ni lugha ya Kipapua nchini Indonesia inayozungumzwa na Wayei. Mwaka wa 2001 idadi ya wasemaji wa Kiyei imehesabiwa kuwa watu 2390 lakini wengi wameanza kuacha lugha yao, yaani Kiyei iko hatarini mwa kutoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kiyei iko katika kundi la Kipapua ya Kusini-Kati.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy