Mshambuliaji

Winga Nani akijaribu kufunga goli kwa kumkwepa beki Philipp Lahm (kulia).
Mshambuliaji (10, jezi nyekundu) kamtoka beki (16, jezi nyeupe) na yupo tayari kupiga shuti kujaribu kufunga. Golikipa naye atajitahidi kuzuioa goli kwa kutokuruhusu mpira usivuke mstari wa goli.

Mshambuliaji (kutoka kitenzi “kushambulia”) ni mchezaji wa nafasi ya mbele anayetakiwa kufunga goli katika michezo mbalimbali kama vile: mpira wa miguu, raga, hoki ya ugani. Hivyo anacheza karibu na goli la timu pinzani akiwa na majukumu makubwa ya kufungia timu yake.

Nafasi yake uwanjani na kazi ndogo ya ukabaji awapo michezoni humaanisha mshambuliaji ndiye wa kufunga magoli mengi zaidi kwa niaba ya timu nzima na wachezaji wenzake.

Mfumo wa kisasa kwa ujumla hutumia mshambuliaji mmoja mpaka watatu; kwa mfano, mfumo uliozoeleka wa 4–2–3–1 hutumia mshambuliaji mmoja.[1][2][3]

  1. Cox, Michael. "FIFA's 289-page Technical Report on the 2010 World Cup – in 15 points", 3 September 2010. Retrieved on 17 August 2013. Archived from the original on 2018-11-04. 
  2. Cox, Michael. "Is Barcelona's alternative shape really a 4–2–4?", 19 March 2010. Retrieved on 17 August 2013. Archived from the original on 2019-02-21. 
  3. Cox, Michael. "Teams of the Decade #5: Roma, 2007", 5 March 2010. Retrieved on 17 August 2013. Archived from the original on 2019-07-26. 

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy