Mtihani

Mtihani ni njia ambayo mtu anapimwa kutokana na alichokisoma au alichofundishwa ili atambuliwe kwamba alielewa au hakuelewa. Au ni kipimo cha maisha kutokana na ulichojifunza.

Katika shule mwanafunzi hupimwa na walimu wake juu ya kile walichomfundisha ili kumjua kama anaelewa au haelewi. Ili tufaulu mitihani tunatakiwa tusome sana na kwa bidii kubwa.

Hivyo mitihani yaweza kuwa migumu au rahisi kutokana na mwanafunzi mwenyewe: kama huwa hajisomei ataiona migumu na kama anajisomea ataiona rahisi hata kama mwalimu alitunga migumu kiasi gani. Kama tujuavyo, lengo la mtihani kwa mwanafunzi ni kumpima kile alichojifunza kutoka chanzo cha mafunzo yake, baada ya kipimo hicho ndipo mwanafunzi anaweza kufanyiwa tathmini ya kumjua kama anafaa kwa lipi na hafai kwa lipi.


From Wikipedia, the free encyclopedia ยท View on Wikipedia

Developed by Tubidy