Ofisa

Ofisa (pia: afisa, kutoka Kiingereza: officer) ni mtu mwenye cheo katika ofisi au katika mfumo wa shirika fulani. Neno latumiwa hasa kwa wanajeshi wa vyeo vyenye mamlaka juu ya wanajeshi wa kawaida.

Katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania vyeo vya maofisa vimepokewa kutoka jeshi la kikoloni vikifuata mfumo wa jeshi la Uingereza.

Maofisa hutofautishwa baina ya wenye kamisheni (ambavyo ni vyeo vya juu zaidi) na maafisa wa ngazi za chini.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy