Waakie

Waakie (pia Wamosiro, kutokana na jina la ukoo mmojawapo) ni kabila dogo la watu wa Tanzania wanaoishi upande wa magharibi wa Mkoa wa Arusha.

Mwaka 2000 walihesabiwa kuwa 5,268 [1].

Waakie, kama makabila mengine ya wawindaji wa Kenya na Tanzania, wanaitwa pengine Wadorobo au Wandorobo.

Wengi wao hawatumii tena lugha yao, Kiakie, bali Kimasai na Kiswahili[1][2][3]

  1. UNESCO Communication and Information: Asie
  2. "Waakie". Wiki Du Học. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-01-13. Iliwekwa mnamo 2024-01-13.
  3. UNESCO Communication and Information: Asie

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy