Wakara

Wakara ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi hasa katika Mkoa wa Mwanza, wilaya ya Ukerewe, hususan katika kisiwa cha Ukara.

Kutokana na uhaba wa ardhi uliosababishwa na ongezeko la kasi la idadi ya watu, Wakara wengine wamelazimika kuhama kisiwa hicho. Kwa sasa wanapatikana kwa wingi katika kisiwa cha Ukerewe na wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, na Chato Mkoa wa Geita[1]

Hadi kufikia mwaka 1987 idadi ya Wakara walikuwa kwa makadirio ya jumla ya 86,000.

  1. "Wanawake wanaotakaswa baada ya kuzaa pacha Tanzania", BBC News Swahili, iliwekwa mnamo 2024-01-13

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy