Arithropodi

Arithropodi
Maumbile ya mdudu
Maumbile ya mdudu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda
Ngazi za chini

Arthropodi ni kundi kubwa la wanyama wenye mwili wa pingili na miguu ya kuunga wasio na ugwe wa mgongo. Mifano ni wadudu, nge, buibui au kaa. Katika uainishaji wa kisayansi wamejumlishwa katika faila ya Arthropoda.

Wote huwa na kiunzi cha nje kinachoundwa na khitini.

Spishi nyingi ni ndogo, hata chini ya mm 1 lakini spishi kadhaa ni kubwa sana, hadi zaidi ya m 1. K.m. kaa wa Japani anaweza kufikia uzito wa kilogramu 15-20. Faila hii ina spishi nyingi sana zinazopatikana kila sehemu ya dunia. Vifundo vya arithropodi ni kama vipashio vilivyounganishwa kuleta mtiririko wa mwili wao.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy