Atlas (milima)

milima ya atlas

Kwa matumizi tofauti ya jina hili tazama Atlas (maana)

Safu za milima ya Atlas.

Milima ya Atlas (kwa Kiberber: Idurar n Watlas; kwa Kiarabu: جبال الأطلس‎, jibaal al-atlas) ni safu ya milima kunjamano katika Afrika ya kaskazini-magharibi. Ina urefu wa takriban kilomita 2,400 kuanzia Moroko kwa kuvukia Algeria hadi Tunisia. Milima ya Atlas hutenganisha pwani ya Atlantiki na Mediteranea kutoka jangwa la Sahara.

Mwinuko wa juu ni Jebel Toubkal nchini Moroko inayofikia mita 4,167 juu ya UB.

Wakazi wa milima hii ni hasa makabila ya Waberber.

Jina la milima hii linatokana na mmoja wa miungu ya Ugiriki ya Kale, Atlas.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy