Bendera ya Tanzania

Bendera ya Tanzania.
Bendera ya Zanzibar baada ya mapinduzi mwaka 1964
iliyotangulia kuundwa kwa bendera ya Tanzania.
Bendera ya Jamhuri ya Tanganyika tangu mwaka 1961 hadi 1964 iliyotangulia kuundwa kwa bendera ya Tanzania.

Bendera ya Tanzania ni ya mstatili unaokatwa pembe kwa pembe na kanda nyeusi yenye milia za njano kandokando[1].

Pembetatu ya juu ina rangi ya majani, pembetatu ya chini ni ya buluu.

Matumizi ya bendera inahifadhiwa chini ya sheria ya "The National Flag and Coat of Arms Act, 15-1971"[2].

  1. National Flag Archived 27 Septemba 2018 at the Wayback Machine., tovuti rasmi ya serikali ya Tanzania, iliangaliwa Desemba 2018
  2. Act to prescribe the National Flag and Coat of arms.. Archived 27 Oktoba 2021 at the Wayback Machine., tovuti ya serikali ya Tanzania, iliangaliwa Desemba 2020

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy