Biolojia ni somo kubwa mno lenye matawi, mada na masomo mengi. Miongoni mwa mada muhimu zaidi kuna kanuni unganishi tano ambazo zinasemekana kuwa misingi yenye hakika na dhahiri ya biolojia ya kisasa:[2]
biolojia ya molekuli huchunguza kuathiriana changamani kwa mifumo ya biolojia ya molekuli, biolojia ya seli huchunguza kijenzi msingi cha maisha yote, seli;
ikolojia huchunguza jinsi viumbehai kadhaa huathiriana na kushirikiana na mazingira yao.[3]
Lugha ya kisayansi katika biolojia inatumia maneno mengi ya asili ya Kigiriki na Kilatini. Lugha nyingi zimeingiza maneno haya tu katika msamiati wao; katika lugha kadhaa wataalamu wametafsiri sehemu ya maneno haya kwa lugha zao lakini kwa ujumla sehemu kubwa na majina ya kisayansi hufuata utaratibu wa Kigiriki na Kilatini.
Wataalamu wengi huona ya kwamba viumbehai vyote hugawiwa katika sehemu au milki kubwa tatu: