Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki

Ramani ya Afrika ya Mashariki inayoonesha volkeno kadhaa (pembetatu nyekundu) na pembetatu ya Afar - eneo la kuachana kwa bamba la Uarabuni na bamba la Afrika linalojipasua hapa kuwa bamba la Afrika ya Kinubia na la Afrika ya kisomalia.

Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki (Kiing. East African Rift Valley) ni maumbile ya kijiolojia yanayoanza katika Mashariki ya Kati na kuendelea hadi Msumbiji. Ni kati ya maajabu makubwa ya dunia. Ufa huu ulitengenezwa miaka milioni 25 iliyopita kutokana na mwendo wa mabamba ya gandunia ya Afrika na Uarabuni.[1] Mwendo huu umesababisha pia farakano ndani ya bamba la Afrika na wataalamu huamini kuwa Afrika ya Mashariki iko katika mwendo wa kuachana na Afrika kwa jumla.[2]

  1. https://academic.oup.com/astrogeo/article/46/2/2.16/216710
  2. https://timesofindia.indiatimes.com/travel/destinations/africa-is-slowly-breaking-into-two-continents/as69465241.cms#:~:text=The%20continent%20of%20Africa%20is,the%20side%20of%20the%20continent.&text=The%20East%20African%20Rift%20Valley,Gulf%20of%20Aden%20to%20Zimbabwe.

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy