British Kolumbia








British Kolumbia

Bendera

Nembo
Nchi Bendera ya Kanada Kanada
Mji mkuu Victoria
Eneo
 - Jumla 944,735 km²
Tovuti:  http://www.gov.bc.ca/
Ziwa Shuswap, British Kolumbia

British Kolumbia (kwa kifupi huitwa B.K.) ni jimbo la Kanada upande wa Bahari Pasifiki lililopo kati ya Marekani bara na Alaska.

Ni mmoja kati ya majimbo makubwa ya Kanada yenye kilomita za mraba zipatazo 944,735.

Kunako mwaka wa 2001, idadi ya wakazi ilikuwa 3,907,738. Kunako mwaka wa 2005, iliaminika ya kwamba idadi ya watu imefikia 4,220,000.

Mji mkuu wa British Kolumbia ni Victoria. Mji mkubwa katika British Kolombia ni Vancouver ambao una wakazi wapatao milioni 2 ndani yake. Miji mingine mikubwa imejumlishwa na Kelowna, Abbotsford, Kamloops, Nanaimo, na Prince George.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy