Cambridge | |
Mahali pa mji wa Cambridge katika Marekani |
|
Majiranukta: 42°22′25″N 71°6′38″W / 42.37361°N 71.11056°W | |
Nchi | Marekani |
---|---|
Jimbo | Massachusetts |
Wilaya | Middlesex |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 101,388 |
Tovuti: www.cambridgema.gov |
Cambridge ni mji wa Marekani katika jimbo la Massachusetts ambayo ni sehemu ya rundiko la jiji la Boston. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mnamo mwaka wa 2007, mji una wakazi wapatao 100,000 wanaoishi katika mji huu. Mji upo m 12 kutoka juu ya usawa wa bahari.
Mji huu uliundwa mwaka 1631 na wakoloni Waingereza kwa jina la "Newe Towne" (mji mpya) kando la Boston. Mwaka 1636 chuo chake cha kwanza kilianzishwa na kutokana na chuo hiki jina la mji likabadilishwa kuwa "Cambridge" kwa heshima la Chuo Kikuu cha Cambridge katika Uingereza.
Leo hii Cambdridge wa Massachusetts inajulikana hasa kutokana na vyuo viwili mashuhuri ambavyo ni Chuo Kikuu cha Harvard na Chuo cha Teknolojia cha Massachusetts (Massachusetts Istitute of Technology MIT).