Casablanca

Casablanca (Kihispania "nyumba nyeupe",tamka kasablanka, ar.| ad-Dār al-Bayḍā’) ni mji mkubwa zaidi nchini Moroko. Ni mji wa bandari uliopo kwenye magharibi ya nchi mwambaoni wa Bahari Atlantiki. Pia ni mju mkubwa kabisa wa nchi za Maghrib na kati ya miji muhimu zaidi kwenye bara la Afrika.

Casablanca ina bandari kubwa ya Moroko[1] ikiwa ni pia kitovu cha benki kubwa za nchi hii. Kufuatana na sensa ya 2012 idadi ya wakazi ilizidi milioni nne katika wilaya yake. Hivyo inatazamiwa kama mji mkuu wa kiuchumi ilhali mji mkuu wa kisiasa ni Rabat.

  1. "Discovering Casablanca". Africa-ata.org. Iliwekwa mnamo 17 Aprili 2011.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy