Charles III (alizaliwa 14 Novemba 1948 kama Charles Philip Arthur George katika Buckingham Palace, London) ni mfalme wa Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire ya Kaskazini tangu tarehe 8 Septemba 2022. Alipokea cheo hicho kutokana na kifo cha mama yake Malkia Elizabeth II[1].
Alirithi pia cheo cha ufalme wa nchi huru 14 zinazoitwa Commonwealth Realms:
Yeye pia ni mkuu wa Jumuiya ya Madola, bwana wa maeneo yaliyopo chini ya Taji la Uingereza na mkuu wa kidunia wa Kanisa Anglikana nchini Uingereza.