Delaware

Sehemu ya Jimbo la Delaware








Delaware

Bendera

Nembo
Nchi Bendera ya Marekani Marekani
Mji mkuu Dover
Eneo
 - Jumla 6,447 km²
 - Kavu 5,060 km² 
 - Maji 1,387 km² 
Tovuti:  http://delaware.gov/
Ramani ya Delaware

Delaware ni jimbo la kujitawala la Maungano ya Madola ya Amerika au Marekani. Iko kwenye pwani ya Atlantiki upande wa mashariki wa Marekani bara. Imepakana na majimbo ya Pennsylvania, Maryland na kwa kilomita chache pia na New Jersey.

Mji mkuu ni Dover lakini mji mkubwa ni Wilmington.

Jina la jimbo linatokana na mto Delaware na hori ya Delaware ambavyo vyote viliitwa kwa heshima ya kabaila Mwingereza De La Warr mnamo mwaka 1600.

Delaware ni jimbo dogo lenye eneo la km² 6,452 na wakazi 783,600 pekee. Kati ya majimbo ya Marekani ni jimbo lenye mapato ya juu kwa kila raia. Sheria zake za kodi ya mapato ni nafuu, hivyo makampuni mengi yamepeleka ofisi zake hapa. Vinginyevyo uzalishaji ni hasa mazao ya kilimo pamoja na ufugaji wa kuku.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy