Dini rasmi

Dini rasmi ni dini ambayo imetangazwa na nchi fulani kuwa yake kwa namna ya pekee. Kiasi ambacho dini hiyo inapata sapoti ya sheria, serikali n.k. inategemea kwa kawaida katiba ya nchi.

Si lazima serikali iwe chini ya mamlaka ya dini hiyo, wala kufuata masharti yake yote, wala kwamba uongozi wa dini uwe chini ya serikali au kwamba serikali iwe chini ya viongozi wa dini.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy