Ibadan

Mahali pa Ibadan katika jimbo la Oyo nchini Nigeria

Ibadan (kwa Kiyoruba Ìbàdàn, kirefu (Ìlú) Ẹ̀bá-Ọ̀dàn, (mji kwenye) ombwe la mbuga) ni mji mkubwa wa tatu wa Nigeria wenye wakazi 3,800,000 (kadirio 2007) na wengi wao ni Wayoruba. Ni mji mkuu wa jimbo la Oyo.

Uko katika Nigeria ya kusini-magharibi, takriban kilometa 125 kutoka Lagos.

Kihistoria ulikuwa kitovu cha Nigeria yote ya magharibi ikiwa makao makuu ya jimbo la magharibi baada ya uhuru wa nchi.

Mji ulianzishwa mwaka 1829 kama makao makuu ya wafalme wa Wayoruba.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy