Indeed

Indeed

Indeed ni tovuti ya kutafuta kazi iliyoanzishwa mnamo Novemba 2004. Ni kampuni tanzu ya kampuni ya Japani ya Recruit Co. Ltd. yenye makao makuu Austin, Texas na Stamford, Connecticut na ofisi nyingine katika nchi kadhaa duniani.[1]

Indeed hivi sana inapatikana kwenye nchi 60 duniani na kwa lugha 28. Mnamo Oktoba 2010, Indeed.com iliipiku Monster.com na kuwa tovuti yenye watumiaji wengi zaidi nchini Marekani.[2]

Tovuti hii inakusanya nafasi za kazi toka kwenye maelfu ya tovuti. Mwaka 2011, Indeed ilianza kuruhusu waomba kazi kutuma maombi moja kwa moja kwenye tovuti yake [3] na pia kuhifadhi maelezo binafsi ya waomba kazi.[4]

  1. "Indeed announces plans for several hundred new Stamford jobs", StamfordAdvocate. 
  2. "Indeed Slips Past Monster, Now Largest Job Site By Unique Visitors". Iliwekwa mnamo Desemba 9, 2010.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "New Feature: Indeed Apply". Resfly Blog. Resfly. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Februari 23, 2012. Iliwekwa mnamo Februari 21, 2012. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)
  4. Zappe, John (Septemba 14, 2011). "Indeed Makes it Official and Launches Resume Search". ere.net. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-09-23. Iliwekwa mnamo Januari 12, 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy