Kenya

Jamhuri ya Kenya
Kaulimbiu ya taifa: "Harambee"
Wimbo wa taifa: "Ee Mungu Nguvu Yetu"
Mahali pa Kenya
Mahali pa Kenya
Ramani ya Kenya
Ramani ya Kenya
Mji mkuu
na mkubwa nchini
Nairobi
1°16′ S 36°48′ E
Lugha rasmi
Lugha za taifaKiswahili
SerikaliJamhuri
 • Rais
 • Makamu wa Rais
 • Spika wa Seneti
 • Spika wa Bunge
 • Jaji Mkuu
William Ruto
Rigathi Gachagua
Amason Kingi
Moses Wetangula
Martha Koome
Eneo
 • Eneo la jumlakm2 580 367[1]
 • Maji (asilimia)2.3
Idadi ya watu
 • Kadirio la 202357 052 004[1]
 • Sensa ya 201947 564 296[2]
Pato la taifaKadirio la 2023
 • JumlaPunguko USD bilioni 112.749[3]
 • Kwa kila mtuPunguko USD 2 187[3]
Pato halisi la taifaKadirio la 2023
 • JumlaOngezeko USD bilioni 338.964[3]
 • Kwa kila mtuOngezeko USD 6 576[3]
Maendeleo (2022)Ongezeko 0.601[4] - wastani
SarafuShilingi ya Kenya
Majira ya saaUTC+3
(Afrika Mashariki)
Muundo wa tarehesiku/mwezi/mwaka
Upande wa magariKushoto
Msimbo wa simu+254
Msimbo wa ISO 3166KE
Jina la kikoa.ke


Kenya, kirasmi Jamhuri ya Kenya, ni nchi iliyoko Afrika Mashariki katika ikweta, kando ya Bahari ya Hindi. Kenya imepakana na Ethiopia upande wa kaskazini, Somalia upande wa kaskazini mashariki, Tanzania upande wa kusini, Uganda na Ziwa Viktoria upande wa magharibi, kisha Sudan Kusini upande wa kaskazini magharibi. Mazingira na tabianchi za Kenya ni anuwai sana; nchini kuna mbuga mbalimbali wanamoishi aina elfu kadhaa za wanyamapori, milima ambayo imefunikwa na theluji (kwa mfano: Mlima Kenya, chanzo cha jina “Kenya”), misitu mikubwa mno, maeneo ya kilimo, halijoto wastani za Bonde la Ufa, na majangwa ya Chalbi na Nyiri. Nchi hiyo anuwai ina watu milioni 47.6 kwa mujibu wa sensa ya 2019.[2] Kwa hivyo, Kenya ni nchi ya 28 kwa idadi ya watu duniani, na ya 7 kwa idadi ya watu barani Afrika. Mji mkuu na mkubwa nchini ni Nairobi, lakini Mombasa ni mji mashuhuri pia, ikiwa mji kongwe na bandari kuu iliyoko kwenye Kisiwa cha Mombasa. Miji mingine ni Nakuru, Ruiru, Eldoret, na Kisumu.

  1. 1.0 1.1 "Kenya". The World Factbook (kwa Kiingereza) (toleo la 2024). Shirika la Ujasusi la Marekani. Iliwekwa mnamo 30 Machi 2024.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 "2019 Kenya Population and Housing Census Volume IV: Distribution of Population by Socio-Economic Characteristics". Kenya National Bureau of Statistics. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 Juni 2020. Iliwekwa mnamo 24 Machi 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 "World Economic Outlook Database, October 2023 Edition. (Kenya)". IMF.org. International Monetary Fund. 10 Oktoba 2023. Iliwekwa mnamo 13 Oktoba 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Human Development Report 2023/24" (PDF) (kwa Kiingereza). Mradi wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa. 13 Machi 2024. uk. 289. Iliwekwa mnamo 13 Machi 2024.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy