Kiambishi awali

Kiambishi awali ni kipande cha neno au mofimu tegemezi inayokaa kabla ya mzizi wa neno. Kwa mfano, neno "anavyolimiwa" mzizi wake ni Lim, na shina hapo ni Lima. Viambishi awali vinavyofanyakazi ni kama ifuatavyo:

  • A = inaonesha kiambishi awali nafsi ya tatu umoja kiwakilishi cha ngeli ya YU-AWA
  • NA = inaonesha kiambishi awali njeo wakati uliopo
  • VYO = Inaonesha kiambishi awali ureshi wa mtenda

  • LIM = Mzizi wa neno

  • IW = Kiambishi tamati (Kauli ya kutendewa)

  • A= Kiambishi kinachodokeza irabu tamati yakinifu

Hiyo ndiyo dhana ya kutambua viambishi awali katika tungo.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy