Kiashiria cha Maendeleo ya Watu

World map
Ramani ya nchi kulingana na maendeleo (kutokana na data za 2022, ilichapishwa mnamo 2024).
  •      ≥ 0.950
  •      0.900–0.950
  •      0.850–0.899
  •      0.800–0.849
  •      0.750–0.799
  •      0.700–0.749
  •      0.650–0.699
  •      0.600–0.649
  •      0.550–0.599
  •      0.500–0.549
  •      0.450–0.499
  •      0.400–0.449
  •      ≤ 0.399
  •      Hakuna data

Kiashiria cha Maendeleo ya Watu (Kiingereza: Human Development Index; kifupi: HDI) ni namba ya takwimu ambayo inaashiria ubora wa elimu, matarajio ya muda wa kuishi, na pato kwa kila mtu na hutumika ili kuweka nchi katika safu nne za maendeleo. Nchi hufanikisha kiashiria bora ikiwa na elimu bora, muda mrefu wa kuishi, na pato kubwa la wastani.

Kiliendelezwa na mchumi Mpakistani Mahbub ul-Haq kikatumiwa sana na Mradi wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa ili kupima maendeleo.

Safu za maendeleo ni duni (<0.550), wastani (0.550-0.699), juu (0.700-0.799), na juu sana (>0.800).[1]

  1. "Data and statistics readers guide" (kwa Kiingereza). Umoja wa Mataifa. Iliwekwa mnamo 2024-04-12.

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy