Kiikoma

Kiikoma (pamoja na lahaja za Kinata na Kiisenye) ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Waikoma. Mwaka wa 2005 idadi ya wasemaji wa Kiikizu-Nata-Isenye imehesabiwa kuwa watu 36,000, yaani Waikoma 15,000, Wanata 11,500 na Waisenye 9,500. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kiikoma-Nata-Isenye iko katika kundi la E40.


From Wikipedia, the free encyclopedia ยท View on Wikipedia

Developed by Tubidy