Kris Kross

Kris Kross
Kris Kross (Smith upande wa kushoto; Kelly upande wa kulia nyakati za usiku) mnamo 1996
Taarifa za awali
ChimbukoAtlanta, Georgia, Marekani
Miaka ya kazi1991–2001
2013 (kuungana tena)
Studio
Ameshirikiana na
Chris "Daddy Mac" Smith
Chris "Mac Daddy" Kelly (amefariki)

Kris Kross lilikuwa kundi la muziki wa hip hop lililoundwa mwanzoni mwa miaka ya 1990, likiongozwa na James Christopher "Mac Daddy" Kelly (Agosti 11, 1978 – Me 1, 2013) na Christopher "Daddy Mac" Smith (amezaliwa Januari 10, 1979). Kundi linatoka nchini Marekani. Kundi lilitamba sana na kibao chao cha 1992 "Jump", ambacho kilishika nafasi ya kwanza kwenye chati za Billboard Hot 100 kwa majuma manane mfululizo na kutunukiwa platinum.

Kundi lilendelea kupata maplatinum na madhahabu kibwena kwa vibao na maalbamu kama vile "Warm It Up", "Tonight's tha Night" na "Young, Rich & Dangerous". Washirika hawa pia walifahamika sana kwa mtindo wao kuvaa nguo kinyumenyume (mbele nyuma, nyuma mbele).

Urafiki wa James Christopher Kelly na Christopher Smith ulianza tangu wakiwa darasa la kwanza. Vijana hawa waligunduliwa na Jermaine Dupri wa enzi hizo aliyekuwa na miaka 19 - aliwakuta katika Marikiti moja huko mjini Atlanta mnamo mwaka wa 1991.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy