Maji matamu

Maziwa kama hapa ziwa la Davos, Uswisi, mara nyingi hujaa maji matamu.

Maji matamu ni maji yasiyo na chumvi nyingi ndani yake.

Kwa kawaida maji ya mvua, ya mtoni au ziwani huitwa "maji matamu" maana yake ya kwamba kimsingi inafaa kwa kunywa au kumwagilia mimea hata kama mara nyingi inaweza kupatikana na matope au machafuko ndani yake. Kinyume chake ni maji ya chumvi jinsi inavyopatikana baharini au katika maziwa kadhaa.

Kitaalamu maji huitwa "matamu" kama kiwango cha chumvi ndani yake ni chini ya asilimia 0.1 au gramu 1 ya chumvi katika lita ya maji. Kama kiwango cha chumvi kinazidi gramu 1/L kupanda hadi gramu 2/L maji hayafai tena kwa matumizi ya kibinadamu[1].

Chumvi ikizidi maji pia hayafai kwa mimea mengi. Kama maji matamu yana kiasi kikubwa cha bakteria au machafuko ndani yake hayafai kwa matumizi ya kibinadamu moja kwa moja lakini inawezekana kusafishwa kwa njia ya kuchuja.

Sehemu kubwa ya maji matamu yanayopatikana duniani ni theluji na barafu ambayo ni hasa mvua iliyowahi kuganda katika hali ya hewa baridi.

  1. Salinity and drinking water , tovuti ya serikali ya Australia Kusini, iliangaliwa Oktoba 2019

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy